Wednesday, October 18, 2006

MASHAIRI YA MAPENZI

[1]
Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.



[2]
Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.



[3]
Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
Akili yake ya nyani, aruka inagongana.



[4]
Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.



[5]
Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.



Hashil S. Hashil

 

No comments: