Monday, October 16, 2006

UZURI

[1]
Uzuri Wa uso mwema,
Unavuta vitu vyote,
vya macho ya kutazama,
unapopita po pote,
Walakini kwa kupima uzuri wa tabia bora

[2]
uzuri kupita kupita huu
katika hii dunia
nawapa msisahau,
Ni nzuri Wa tabia
Ni johari ya heshima duniani kila mara

[3]
tazama! dunia nzima
Huendeshwa na tabia
kama tabia Si njema,
si ajabu kupotea.
Kitu kilicho adhama ni tabia na busara.

[4]
Kwa kutengeza tabia,
Rai yangu na fikira
Vyuo katika dunia
Vingekuwa na tijara
kwa kuwa nayo daima sera na tabia bora.

No comments: