Monday, October 16, 2006

DUA

[1]
Twakuomba mtukufu.
Asokijana na kufu.
Mola wetu maarufu.
AlIahu alo karima.


[2]
Mikono tumeinua.
Mola wetu watujuwa,
Takabali yetu duwa.
Utupe lililo nawema.


[3]
Mola machozi yatoka.
Hakika ya bubujika,
Tumetubu kwa hakika.
Waja wako tumekoma.


[4]
Rabbi sisi waja wako.
Twatubu twa rudi kwako.
Tutini ya twaa yako.
Tukubaile karima.


[5]
Ya Rabbi tupe Ilimu.
Tupe na njema Fahamu.
Ya kutambua vigumu.
Vya dini yako Karima.


[6]
Utupe matunda yake,
Tuisome tusichoke.
Mola ilimu iweke.
Moyoni mahala pema


[7]
Rabbi ijapo hukumu.
Isiwe kwetu ni ngumu,
Tusiweze kudhulumu.
Tukuche wewe Karima.


[8]
Turuzuku nyingi hima
Isiokuwa na kukoma.
Utupe na kulla jema.
Duniani na kiama.


[9]
Tupe Riziki halali.
iso na uthakili.
Utupe na njema hali
Duniyani na kiyama.


[10]
Tuondoshee laudhiya.
Lilo na kulla baliya,
Utupe liso udhiya.
La-dini yako karima.


[11]
Utupe na kupendana.
Sisi na wetu vijana,
Mapenzi yaso khiyana.
Ya dini yako karima.


[12]
Utupe njema fasaha
iso kuwa najaraha.
Utupe nyingi furaha,
Duniani na kiyama.


[13]
Tutunze mijini mwetu.
Tukidhie deni zetu.
Kabla ya kuja kwetu,
Mjumbe wa mauti mwema.


[14]
Sizi vunde zetu hima,
Tuawini wima wima.
Utujaze yako mema.
Duniani na Kiyama.


[15]
Tubarikie Jalili.
Umriwetu twawili.
Sote na kulia adili.
Afunzae kula jema.


[16]
Kulla ajae na shari.
Waijuwa yake siri
ivunde yake dhamiri.
Asiweze kusimama.


[17]
Rabbi swala na salamu.
Umfikilie hashimu
Na sahaba ze kiramu
Na alo kulla mwema


[18]
Amina Rabbi Amina
Amina Rabbi Amina
Amina Rabbi Amina.
Tukubalie Karima.

 

2 comments:

Anonymous said...

Fantastic, Mungu akujazi kheri. Please hebu angalia hiyo namba 4 iko na typo error.

Anonymous said...

Iko sawa, Tutini means tuko chini :)